You are currently viewing IGP Wambura: Dkt Samia ametutoa kwenye vibanda, katujengea maghorofa

IGP Wambura: Dkt Samia ametutoa kwenye vibanda, katujengea maghorofa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ( (IGP), Camillius Wambura katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan jeshi hilo limepiga hatua kubwa ikiwemo maboresho ya makazi kutoka kwenye vibanda vya mabati hadi nyumba za kisasa za askari hao.

IGP Wambura amesema makazi ya askari yalikuwa katika mazingira magumu ikiwemo kuishi katika vibanda vilivyojengwa kwa mfumo wa mabati mithili ya nyumba za  wavuvi wa samaki.

Wambura amesema hayo leo katika hafla ya kufunga mafunzo ya kozi namba 1/2025/ 2026 ya maofisa na wakaguzi wasaidizi wa Jeshi la Polisi iliyofanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam yaliyohudhuriwa na Dkt Samia.

” Mheshimiwa Rais yale yamejengo ulioyaona pale kwenye slide si kambi za wavuvi, bali ni makazi ya polisi ambayo askari walilala humo na kwenda kulinda raia na mali zao.Majengo hayo yameisha kwa muda mrefu, lakini wewe umeyakataaa.

” Umetoa fedha na kuhakikisha majengo ya kisasa ya makazi ya askari yanajengwa hasa maghorofa, hii imeondoa hata yale makazi ambayo hata wavuvi wasingeweza kukaa.

Amesema ” sisi ni kina nani tusisimulie hadithi hii? Au kina nani tusiokuwa na roho ya shukrani ya kusimulia hadithi hii, mheshimiwa Rais asante sana,” amesema IGP Wambura.

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi, amesema mabadiliko hayo yaliyofanywa na Dkt Samia  yataachaa alama kubwa ndani ya jeshi la polisi na vizazi vijavyo sambamba na kuweka kumbukumbu ndani ya jeshi hilo.

Ameeleza kuwa uongozi wa Dkt Samia umewezesha pia Jeshi la Polisi kupata vyombo mbalimbali vya usafiri, yakiwemo magari ya kisasa sambamba ajira mpya katika jeshi hilo,  upandishaji wa vyeo kwa askari na ujenzi wa vituo vya kisasa vya polisi.