Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amesema biashara kati ya nchi hiyo na Tanzania imeendelea kukua kwa kasi, huku kiwango kikiongezeka kati ya asilimia 20 hadi 25 kwa mwaka 2025.
Amefafanua kuwa hatua hiyo inayodhihirisha kuimarika kwa ushirikiano wa kiuchumi na kunufaisha wananchi wa pande wa Urusi na Tanzania.
Rais Putin ameeleza hayo leo Jumatano Juni 3,2026 wakati mazungumzo na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Ikulu ya Kremlin Rais Putin akieleza kuwa mesema ukuaji huo unaonyesha kuimarika kwa ushirikiano wa kiuchumi na mahusiano ya kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili, yanayoaadhimisha miaka 65 ya uhusiano wa kidiplomasia.
Kiongozi huyo wa Urusi amesema kuwa ongezeko hilo ni hatua muhimu, lakini akasisitiza kuwa bado kuna fursa nyingi za kuongeza biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi.
Rais Putin amezitaja sekta za madini, usafiri na usafirishaji, afya na elimu kuwa miongoni mwa maeneo yenye nafasi kubwa ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.
Naye, Rais Samia amesema ziara yake itaimarisha ushirikiano na kukuza fursa za maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na Urusi.
