You are currently viewing Dkt Samia aitangaza Tanzania katika jukwaa la dunia

Dkt Samia aitangaza Tanzania katika jukwaa la dunia

Rais Dk Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuiweka Tanzania kwenye ramani ya uchumi wa dunia, baada ya kushiriki Jukwaa la 29 la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg nchini Urusi.

Jukwaa hilo limewakutanisha zaidi ya washiriki 24,000 kutoka zaidi ya nchi 140, wakiwemo wakuu wa nchi, wawekezaji na viongozi wa makampuni makubwa duniani.

Kupitia ushiriki huo, Tanzania imepata fursa ya kutangaza vivutio vyake vya uwekezaji katika sekta za madini, nishati, utalii, kilimo na usafirishaji.

Hatua hiyo inaendelea kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha biashara na uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.