Mwenyekiti wa Madereva Bodaboda wa eneo la Machinga Complex, Dodoma, Joseph Mjungu, ameeleza kufurahishwa na uamuzi wa Serikali kusitisha mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa, kwani ndio njia pekee ya kulinda usalama na shughuli zao.
Ameyasema hayo alipozungumza sokoni hapo, baada ya kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi, aliyetaka utoaji wa vibali vya mikutano ya hadhara usitishwe kwa muda.
“Kama kweli Serikali imeona mikutano ya vyama vya siasa inaleta uchochezi, sintofahamu na kuvuruga amani, basi kauli hiyo haina budi kuungwa mkono, na sisi tunaiunga mkono,” amesema Mjungu.
Amesema Watanzania wanakumbuka yaliyotokea Oktoba 29 na kusisitiza kuwa hawataki kuona hali kama hiyo ikijirudia.
