You are currently viewing Makusanyo ya mapato hospitali ya Wilaya Magu yazidi kupaa

Makusanyo ya mapato hospitali ya Wilaya Magu yazidi kupaa

Kamati ya ulinzi na usalama ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu imeeleza kuridhishwa na Mfumo wa kukusanya mapato ya Hospitali ya Wilaya ya Magu (GOT- HOMIS) baada ya kufanikiwa kuongeza makusanyo ya mapato ya hospitali kwa zaidi ya asilimia 100. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Hayo yamejiri mwishoni mwa wiki katika ziara ya Kamati ya ulinzi na usalama Halmashauri ya Wilaya ya Magu iliyoongozwa na mkuu wa wilaya, Joshua Nassari.

Ziara hiyo ililenga kukagua utoaji wa huduma katika hospitali ya Wilaya ya Magu, kukagua majengo mapya ya wodi ya mama na mtoto, wodi ya wanaume na stoo ya dawa.

Wakati wa ziara hiyo mkuu huyo wa wilaya ya Magu, pia alizungumza na wananchi ambao walifika hospitalini hapo kupata huduma za afya ambapo pamoja na mambo mengine walipongeza ubora wa huduma unaotolewa hospitalini hapo

Akizungumza baada ya kukagua utoaji wa huduma hospitalini hapo DC Nassari naye aliwapongeza watoa huduma za afya na kuwasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia misingi ya utumishi katika kutoa huduma.

Aidha, aliwasisitiza watumishi hao wa afya kufanya kazi kwa uweledi na kuzingatia maadili ya kazi hususani lugha na utu katika kutoa huduma.

Leave a Reply