Rais Samia Suluhu Hassan amesema walipa kodi ni nguzo muhimu ya maendeleo ya taifa kutokana na mchango wao katika kukuza uchumi kupitia ulipaji wa kodi.
Rais Samia amesema hayo leo Julai Mosi, 2026 wakati akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Utoaji wa Tuzo ya Rais ya Mlipaji Kodi Bora yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“Tuzo hii inatolewa kwa mara ya kwanza ikiitwa Tuzo ya Rais kwa Mlipaji Kodi Bora, tunapowatunuku leo tunatuma ujumbe kwa walipa kodi wote nchini kwamba serikali inatambua, inathamini mchango wenu katika kulijenga taifa letu,” amesema.
