You are currently viewing Rais Samia: Kulipa kodi ni uzalendo kuelekea kujitegemea

Rais Samia: Kulipa kodi ni uzalendo kuelekea kujitegemea

Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka wafanyabiashara waendelee kulipa kodi, akisema hicho ni kitendo cha kizalendo na kinaipa nchi heshima kuelekea uchumi wa kujitegemea.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Jumatano Julai 1, 2026 alipozungumza katika hafla ya maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na utoaji wa Tuzo za Rais kwa Walipakodi.

“Tunaishi katika zama za mataifa kukubaliana katika biashara na kwa kiasi kikubwa kupungua kwa misaada. Tunaishi katika zama za kuongezeka kwa masharti ya mikopo, wakati huohuo kuna ongezeko la mahitaji ya wananchi,” amesema.

Kwa msingi huo, amesema hatuna budi kujenga uwezo wetu wa ndani kwa kuimarisha ukusanyaji wa mapato ili kujenga uchumi unaojitegemea kwa kiasi kikubwa,” amesema.