Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete leo Jumatano ametembelea Banda la NMB kwenye Maadhimisho ya wiki ya Vijana katika viwanja vya Soko la Uhindini jijini Mbeya.
Kikwete amepokewa na Meneja Mahusiano Idara ya Wateja Binafsi – Luiana Keenja pamoja na Meneja Mauzo Kanda Nyanda
za Juu Ungandeka Mwakatage (katikati).

Benki ya NMB ambayo ni mmoja wa wadhamini wa maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa na sherehe za kitaifa za kuzima Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika Oktoba 14 mwaka huu jijini Mbeya, tayari imekabidhi hundi ya Shilingi Milioni 30.
Katika kipindi cha miaka mitano ambayo mbio za Mwenge wa Uhuru zimefanyika, benki hiyo imetoa udhamini wa Zaidi ya Sh. Milioni 439.

Maadhimisho ya wiki ya vijana duniani yanafanyika kitaifa jijini Mbeya na yanatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 14 mwaka huu siku ambayo pia itaambatana na maadhimisho ya miaka 26 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimua Julius Kambarage Nyerere na uzimaji wa Mwenge wa Uhuru.
