You are currently viewing Rais Samia amuapisha Mwanasheria mkuu wa Serikali
Hamza Johari

Rais Samia amuapisha Mwanasheria mkuu wa Serikali

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemwapisha Hamza Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Johari ameapishwa leo Jumatano, Novemba 5, 20254, Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi.

Johari ameapishwa baada ya kuteuliwa na Rais Samia Novemba 3, 2025, saa chache baada ya Samia kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania.

Johari ameapishwa kuendelea na wadhifa huo baada ya kuwa kuteuliwa kwa mara ya kwanza Agosti 15, 2024 kuchukua nafasi ya Dk Eliezer Feleshi ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Leave a Reply