Rais Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaendeleza maridhiano ya kisiasa nchini kuelekea hatua za maboresho ya Katiba kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Katika kuyatimiza hayo, ameahidi kuendeleza majadiliano na vyama vya siasa ili kujenga mwafaka kuhusu masuala muhimu ya Taifa.`
Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 30, 2026 alipokutana na viongozi wa vyama 18 vya siasa nchini katika mkutano uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Katika hotuba yake, amerejea maridhiano ya Zanzibar, akisema Serikali inaendelea na maandalizi ya hatua zinazofuata za mapitio ya Katiba na kwamba kila hatua itazingatia misingi ya sheria na maslahi mapana ya Taifa.
Aidha, amesema Serikali itaendelea kukutana na viongozi wa vyama vya siasa angalau mara tatu kwa mwaka kwa lengo la kuimarisha mazungumzo, kujenga uelewano na kutafuta suluhu za masuala yanayohusu maendeleo ya nchi.
Mbali na masuala ya siasa, Rais Samia pia amezungumzia hali ya uchumi wa nchi akisema umeendelea kukua kwa asilimia sita mwaka uliopita, huku ukuaji wa asilimia 6.3 ukitarajiwa mwaka huu.
