Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Kijinai katika Matukio ya Ghasia za Wakati na Baadaa ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, imeweka wazi hadidu za rejea itakazokwenda kuzifanyia kazi katika mchakato.
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Shaban Lila ametaja hadidu hizo leo Agosti 24,2026 mbele ya wanahabari akisema ndio uwanda na mipaka ya ambayo tume hiyo itakayokwenda kuifanyia kazi.
Kwa mujibu wa Jaji Lila, Tume itachunguza na kubainia wahusika wa ghasia, namna kila mmoja alivyoshiriki kupanga, kufadhili, kuratibu au kufanya ghasia za wakati Oktoba 29.
Pia, Tume itachunguza matukio mahsusi ikiwemo vifo visivyo kwa kawaida vya watoto na watu wa makundi maalumu na watu waliopotea.
“Tume itachunguza madai ya matumizi ya nguvu kuzidi kiasi dhidi ya taratibu na miongozo iliyowekwa wakati na baada ya uchaguzi mkuu. Pia Tume itachunguza suala lolote ambalo Tume itaona muhimu linaloendana na majukumu ya Tume,” ameeleza Jaji Lila.
