Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa wanne na kuwahamisha wengine. Walioteuliwa ni Salum Hamduni aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga (RAS) ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Alexander Mnyeti ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita. Mnyeti amewahi kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Pia, Stanslaus Nyongo yeye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Nyongo amewahi kuwa Naibu Waziri wa Mipango na Uwekezaji.
Aidha, aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Jumanne Sagini ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa leo Alhamisi, Agosti 27, 2026 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikuli, Bakari Machumu.


