You are currently viewing Mji wa Serikali Dodoma umeongeza tija, kasi huduma kwa wananchi

Mji wa Serikali Dodoma umeongeza tija, kasi huduma kwa wananchi

Kuelekea uzinduzi wa majengo ya wizara na taasisi za Serikali katika Mji wa Serikali Dodoma, unaotarajiwa kufanyika kesho, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Nsubili Joshua, amesema mji huo umerahisisha utendaji kazi wa Serikali kwa kuongeza tija, kurahisisha uratibu wa shughuli za Serikali na kuharakisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Amesema kuwepo kwa wizara na taasisi za Serikali katika eneo moja kumewawezesha watumishi kuratibu shughuli zao kwa urahisi zaidi, kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi na kupunguza urasimu katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

Aidha, amesema mpangilio huo unarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi, huku ukiimarisha uwazi, uwajibikaji na ufuatiliaji wa utekelezaji wa majukumu ya taasisi za umma.

Ameongeza kuwa Mji wa Serikali Dodoma unasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali kupitia matumizi bora ya rasilimali na uboreshaji wa mifumo ya kiutendaji, hatua inayolenga kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.