You are currently viewing NIT yaongeza ndege mbili kuimarisha mafunzo kwa wanafunzi wa kozi za urubani

NIT yaongeza ndege mbili kuimarisha mafunzo kwa wanafunzi wa kozi za urubani

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT_TANZANIA kimeongeza ndege mbili mpya kutoka kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Textron Aviation.

Ndege hizo ni pamoja na Beechcraft G58 Baron na Cessna 172 Skyhawk yenye usajili wa 5H-NID, ambazo zitawezesha mafunzo kwa wanafunzi wanaosomea kozi za urubani katika chuo hicho.

Hatua hiyo inalenga kupanua uwezo wake wa kutoa mafunzo ya anga kupitia uwekezaji wa Serikali katika ndege za mafunzo na programu za urubani pamoja na matengenezo ya ndege.

Aidha, taasisi hiyo imepanua mafunzo ya ufundi wa ndege kwa kuzingatia viwango vya kimataifa, ikiwemo mifumo ya mafunzo ya matengenezo inayohusishwa na Wakala wa Usalama wa Usafiri wa Anga wa Umoja wa Ulaya (EASA).

Hatua hiyo inalenga kuongeza wataalamu wa anga nchini, kupunguza utegemezi wa mafunzo nje ya nchi na kuimarisha uwezo wa Tanzania katika sekta ya usafiri wa anga.