You are currently viewing Watendaji tatueni changamoto za wananchi msisubiri maelekezo- Rais Samia

Watendaji tatueni changamoto za wananchi msisubiri maelekezo- Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka Makatibu Wakuu wa Wizara kutumia mamlaka na nafasi zao kusimamia utendaji wa taasisi zilizo chini yao na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi bila kusubiri kila mara maelekezo kutoka kwa Mawaziri.

Rais Samia amesema kuna changamoto mbalimbali zinazohitaji usimamizi wa karibu, ikiwamo uwepo wa mbolea feki, uuzaji wa mbolea zinazotolewa kwa ruzuku nje ya utaratibu pamoja na vitendo vya ubadhirifu katika baadhi ya vyama vya ushirika vinavyowaathiri wakulima.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo, Novemba 27, 2026, Ikulu ya Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi wateule, wakati akitoa maelekezo kwa Niabu Waziri wa Kilimo mpya, Cecilia Paresso. 

Amesema Makatibu Wakuu wanapaswa kushirikiana na viongozi wa taasisi zilizo chini ya wizara zao kubaini na kushughulikia changamoto hizo ili kuhakikisha wananchi, hususan wakulima, wanapata huduma na haki zao stahiki.

Aidha, amewataka kutobaki katika kusubiri maelekezo ya Mawaziri, bali kutumia uelewa na uzoefu wao katika kusimamia majukumu yao na kubuni njia za kutatua changamoto zinazojitokeza katika sekta wanazozisimamia.