Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limepanga kuanzisha tena safari za moja kwa moja kuelekea Jonannesburg nchini Afrika Kusini.
Kulingana na ATCL, safari hizo ambazo zitakuwa mara tano kwa wiki, zinatarajiwa kuanza Novemba 30, 2024.
Ratiba iliyotolewa na ATCL kwenye ukurasa wake wa X, inaonesha kuwa kutakuwa na ndege ya moja kwa moja kuelekea Johannesburg kuanzia siku ya Jumatatu, Jumatano, Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kila wiki.