Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania imesema kuanzia tarehe 15 Juni 2025 Shirika la Ndege la Flightlink litaanzísha safari za moja kwa moja kutoka Arusha kwenda Nairobi na kurudi.
Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Jumatatu imesema mamlaka kwa kushirikiana na Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji tayari inamalizia kufunga mfumo na kupanga maafisa wa Uhamiaji kwenye kiwanja cha ndege cha Arusha ili kuwezesha safari hizo.
“Mamlaka kwa kushirikiana na wadau wa usafiri wa Anga inaendelea kufanya jitihada za kurahisisha usafiri kupitia viwanja vyake na inapokea maoni ya namna bora ya kuendelea kuboresha huduma kwenye Viwanja vyake,” imesema.