You are currently viewing Baraza Haki za Binadamu laipongeza Tanzania kulinda haki

Baraza Haki za Binadamu laipongeza Tanzania kulinda haki

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (HRC) limeipongeza Tanzania kwa kuonesha mwenendo mzuri wa kulinda haki za binadamu na amani, huku hali hiyo ikitajwa kuzorota katika mataifa mengine, ikiwemo Marekani na Iran.

Pongezi hizo kwa Tanzania, zimetolewa na Kamishna Mkuu wa HRC, Volker Türk, katika hotuba yake, wakati wa ufunguzi wa Kikao cha 61 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika Geneva nchini Uswizi.

Katika hotuba hiyo, Türk ameitaja hatua ya Serikali ya Tanzania kuunda Tume ya Uchunguzi wa Vurugu wakati wa Uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, akisema inaonyesha dhamira ya nchi kushughulikia changamoto kwa kuzingatia misingi ya haki na utawala wa sheria.

Hata hivyo, Kamishna huyo, amesema katika baadhi ya nchi kumekuwa na mwenendo mbaya wa haki za binadamu, akiikosoa Marekani kutokana na operesheni dhidi ya wahamiaji haramu zinazodaiwa kukiuka misingi ya haki za binadamu na Iran kwa ukandamizaji wa waandamanaji.

Leave a Reply