Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imeridhia mapendekezo ya marekebisho ya kanuni za uteuzi wa wagombea uongozi katika vyombo vya dola ikiwemo kuweka ukomo wa vipindi viwili vya miaka mitano kwa nafasi za ubunge/uwakilishi na udiwani wa viti maalum wanawake.
Taarifa ya kamati hiyo iliyotolewa leo Machi 11, 2025 na Katibu wa NEC Organaizesheni, Issa Haji Ussi (GAVU) imesema ukomo huo utaanza kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.

Hayo yamejiri katika kikao cha halmashauri hiyo kilichofanyika jana tarehe 10 Machi, 2025 jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Rais Samia Suluhu Hassan.
“Katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imepokea na kujadili agenda kuu mbili kama zifuatazo:- Mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi wa Wagombea uongozi katika vyombo vya Dola toleo la 2022 na Rasimu ya Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa 2025- 2030,” imesema taarifa hiyo.
Vilevile, Halmashauri Kuu ya CCM ya Talfa imepitisha Kauli Mbiu rasmi kwa ajili ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2025 isemayo; “KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE”
“Kauli mbiu hiyo inaakisi dhamira ya Chama ya kuendeleza juhudi za ujenzi wa Taifa lenye maendeleo jumuishi, mshikamano wa kitalfa na ustawi wa watu wenye kujali UTU.