You are currently viewing Dk. Bashiru aanika mazito utendaji wa Samia

Dk. Bashiru aanika mazito utendaji wa Samia

Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amemtaja Mgombea urais wa chama hicho, Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa kiongozi mwenye utulivu, ujasiri na umakini wa pekee.

Msingi wa kauli hiyo ya Dk Bashiru ni kile alichofafanua, kwa kuwa alikuwa sehemu ya vikao vya uamuzi serikalini, ameshuhudia ujasiri huo wa Dkt Samia alivyoivusha Tanzania salama, baada ya msiba wa Rais wa tano, hayati John Magufuli. 

Dkt Bashiru ameyasema hayo leo, Jumanne Septemba 9, 2025 alipozungumza katika mkutano wa kampeni za urais za CCM, zilizofanyika katika Uwanja wa Bombadier Singida Mjini.

Katibu Mkuu kiongozi huyo mstaafu amesema Dkt Samia ameingia madarakani kukiwa na hali ngumu ya kisiasa na kiuchumi, lakini alifanikiwa kuivusha nchi bila kuathirika kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na nchi nyingine.

Hali ya wakati huo, amesema ilihitaji utulivu, umakini na ujasiri na kwa kuwa Dkt Samia ana sifa zote hizo na inatosha kumpa nafasi nyingine ya kuiongoza Tanzania kwa miaka mitano.

“Huyu kiongozi wetu, ana utulivu wa aina yake, ana ujasiri na umakini wa aina yake, kwa sababu hali hiyo ilihitaji utulivu, umakini na ujasiri na nakubaliana na Kishoa, sifa hiyo pekee inatosha kumuongezea nafasi atuongoze,” amesema.

Leave a Reply