You are currently viewing Dk. Biteko asisitiza Watanzania kupiga kura  uchaguzi serikali za mitaa

Dk. Biteko asisitiza Watanzania kupiga kura  uchaguzi serikali za mitaa

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko  amewahimiza  Watanzania kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Dk. Biteko ametoa rai hiyo  leo Novemba 25,2024 akiwa mkoani Geita ambapo amesema uchaguzi huo ni muhimu hususan kwa ukuzaji wa demokrasia nchini.

“Naomba Watanzania wote waliojiandikisha kwenye Daftari la Kupiga Kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa  katika maeneo yao wajitokeze kupiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi wao,” amesema Dkt. Biteko.

Amesisitiza “ Viongozi hawa ndio msingi katika nchi yetu, viongozi hawa ndio wanajua watu wanaishije, wana shida gani na watafanya nini kutatua shida hizo. Ni muhimu wote kushiriki kuchagua viongozi tunaowataka,” amesisitiza.

Aidha, Dk. Biteko amebainisha kuwa kupiga kura ni haki ya kila  Mtanzania mwenye sifa hivyo watu wote wenye sifa wajitokeze kupiga kura ifikapo Novemba 27, 2024. 

Leave a Reply