You are currently viewing Dkt. Samia ampokea Rais wa Misri El-Sisi Ikulu Dar es Salaam

Dkt. Samia ampokea Rais wa Misri El-Sisi Ikulu Dar es Salaam

Rais Samia Suluhu Hassan, leo Julai 18, 2026 amempokea Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fattah El-Sisi aliyewasili Nchini kwa ziara ya Kitaifa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, baada ya mapokezi hayo viongozi hao watafanya mazungumzo rasmi yatakayolenga kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Misri pamoja na kupanua ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwamo biashara, uwekezaji, kilimo, nishati, maji, afya, elimu na miundombinu.

Kadhalika, Rais Samia na Rais El-Sisi watashiriki Jukwaa la Biashara la Tanzania na Misri litakalowakutanisha Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka mataifa hayo mawili kwa lengo la kujadili fursa za biashara na uwekezaji.

Ziara hiyo inatarajiwa kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo kati ya Tanzania na Misri na kufungua fursa mpya za biashara na uwekezaji kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili.