You are currently viewing  Dkt Samia: Kuwe na haki, usawa ulipaji kodi

 Dkt Samia: Kuwe na haki, usawa ulipaji kodi

Kilio cha baadhi ya wafanyabiashara kuhusu mfumo wa haki na usawa katika ulipaji wa kodi, kinakwenda kupata muarobaini, baada ya Tume ya Tume ya Rais ya Kutathmini Maboresho ya Mfumo wa Kodi kutoa mapendekezo ya kukabiliana na changamoto hiyo.

Hayo yamebainishwa leo Jumatano Machi 18, 2026 wakati Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya Tume ya Rais ya Kutathmini Maboresho ya Mfumo wa Kodi nchini. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Baada ya kupokea ripoti hiyo, Dkt Samia amesema: “ndugu zangu nimesikiliza kwa makini mapendekezo yaliyotolewa na Tume, ambapo pamoja na mambo mengine yanajielekeza kuboresha sera na sheria za kodi, mazingira ya uwekezaji na biashara, mifumo ya Tehama, kitaasisi ya ukusanyaji mapato na maduhuli na utatuzi wa migogoro ya kikodi,”

“Kwa ujumla tukiyatekeleza vyema, mapendekezo yaliyotolewa yatatuelekeza katika mfumo wa haki na usawa katika ulipaji wa kodi. Kuna malalamiko mengi, kuna wengine wanalipa sawa, wengine wana vichochoro vya kupita na kulipa kodi kidogo,” ameeleza Dkt Samia.

Kwa mujibu wa Rais Dkt Samia, kuna wengine wanapitisha bidhaa kwa magendo na kusababisha uwanja wa soko kutokuwa sawa, hivyo mapendekezo ya Tume yanaeleza namna ya kukabiliana na changamoto hizo.

“Mapendekezo haya yatatuyelekeza huko, kuwa na kodi ya haki na usawa, kwa kila mfanyabiashara kwa kiwango cha biashara anayoifanya, sio wengine wakubwa, au wengine hawalipi aahahha…,” amesisitiza Dkt Samia.

Rais Samia aliunda Tume Kutathmini Maboresho ya Mfumo wa Kodi hiyo Oktoba 4, 2024 ikiwa imepita miaka 30 tangu kuundwa kwa tume kama hiyo na Edwini Mtei (Marehemu).

Leave a Reply