You are currently viewing Wagombea urais wafungwa miaka 10 kwa ufisadi

Wagombea urais wafungwa miaka 10 kwa ufisadi

Mahakama nchini Algeria imewahukumu kifungo cha miaka 10 gerezani wagombea watatu wa urais baada ya kuwatia hatiani kwa makosa ya ufisadi.

Mfanyabiashara Saida Neghza, waziri wa zamani Belkacem Sahli na Abdelhakim Hamadi ni miongoni mwa watu 70 waliohukumiwa kwenda jela hapo jana Jumatatu ambapo wengine walihukumiwa kifungo miaka mitano na minane.

Watatu hao walikuwa wanataka kuwania urais kwenye uchaguzi wa Septemba, lakini wote walizuiwa na mamlaka za uchaguzi na badala yake kushitakiwa kwa kujaribu kununuwa saini za watu wa kuwaunga mkono.

Miongoni mwa walioshitakiwa walikuwa watoto watatu wa kiume wa mfanyabiashara Saida Neghza.

Wote wanakanusha kuhusika na ufisadi wowote na badala yake wanaelezea hukumu dhidi yao kuwa ni adhabu ya kumkosowa Rais Abdelmajid Tebboune kwa uongozi wake mbaya.

Leave a Reply