You are currently viewing Dkt Samia: Nitajenga hospitali maalumu ya mama na mtoto Kurasini

Dkt Samia: Nitajenga hospitali maalumu ya mama na mtoto Kurasini

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Katika kusogeza huduma karibu za uzazi, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema atajenga hospitali maalumu ya mama na mtoto, eneo la Kilwa Road Kurasini, ili kurahisisha upatikanaji wa matibabu.

Ujenzi huo ni mwendelezo wa uboreshaji wa sekta ya afya katika hospitali ya polisi iliyopo katika hilo, wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam.

Ameeleza hayo leo Alhamisi, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya kozi namba 1/2025/ 2026 ya maofisa na wakaguzi wasaidizi wa Jeshi la Polisi iliyofanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.

“Wakati nikinongo’na ndani kule na IGP, alinieleza haja kuwa na hospitali maalumu ya kina mama na watoto, pale katika hospitali ya Kilwa Road. Nami nimemuhakikishia hospitali umeipata, hospitalia umeipata na nakusudia itajengwa hivi karibuni,” amesema.