You are currently viewing Haya hapa matokeo darasa la saba 2025, ufaulu waongezeka
Profesa Said Ally Mohamed

Haya hapa matokeo darasa la saba 2025, ufaulu waongezeka

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) 2025 leo, Jumatano Novemba 5, 2025, ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.93 ikilinganishwa na mwaka 2024.

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Ally Mohamed, jumla ya watahiniwa 1,172,279 walifanya mtihani huo, wakiwemo wavulana 535,138 (45.65%) na wasichana 637,141 (54.35%).

Kati yao, 937,581 sawa na asilimia 81.80 wamefaulu kwa kupata madaraja A, B na C, ikilinganishwa na asilimia 80.87 mwaka 2024. Wavulana waliofaulu ni 429,104 (82.51%) na wasichana 508,477 (81.21%).

Aidha, ubora wa ufaulu umeimarika ambapo watahiniwa 422,923 (36.90%) wamepata madaraja ya juu (A na B), kutoka asilimia 35.83 mwaka 2024 — ongezeko la asilimia 1.07.

Tazama matokeo kamili hapa; https://matokeo.necta.go.tz/results/2025/psle/psle.htm

Leave a Reply