Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Anda Filip, ameipongeza Tanzania kwa hatua iliyopiga katika kuongeza ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi, akisema uzoefu wa Tanzania unaweza kuwa somo kwa mataifa mengine katika kujenga mifumo jumuishi ya kufanya maamuzi.
Akizungumza katika mahojiano wakati wa Mkutano wa 153 wa IPU unaofanyika Arusha, Filip amesema anavutiwa na uwakilishi wa wanawake katika Bunge la Tanzania, ambao umefikia karibu asilimia 40, akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha wanawake wanapata nafasi ya kushiriki kikamilifu katika michakato ya kisiasa na maamuzi ya kitaifa.
Filip amesema Tanzania, kupitia Dira ya Maendeleo 2050, ina fursa ya kuimarisha ushiriki wa wanawake na vijana katika kujenga na kutekeleza ajenda za maendeleo ya muda mrefu, ili kuhakikisha vipaumbele vya taifa vinaendelea kutekelezwa na vizazi vijavyo bila kutegemea mabadiliko ya awamu za uongozi.
#IPU153Tanzania
