You are currently viewing Kilichombeba Dk. Samia kuwa kinara afya ya mama na mtoto Afrika
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo

Kilichombeba Dk. Samia kuwa kinara afya ya mama na mtoto Afrika

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema hatua ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuteuliwa kuwa kinara wa afya ya mama na mtoto katika Umoja wa Afrika (AU), imetokana na kufanya vema zaidi katika huduma hizo zaidi na mataifa mengine.

Balozi Kombo ametoa kauli hiyo leo, Jumatatu Februari 16, 2026 wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ziara za Rais Dkt Samia nje ya nchi, hafla iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Amesema Dkt Samia aliwahi kupendekeza mtandao wa WhatsApp utumike kujua alipo mjamzito, nyakati anazopatwa na uchungu, anafikiwaje na kituo kilichopo karibu naye kina huduma zipi na kama kuna shida apelekwe wapi.

Pendekezo hilo, amesema linatumika na nchi saba barani Afrika na ndio maana amepewa nafasi ya kuwa kinara. Pia, hilo limepunguza vifo vya mama na mtoto.

Leave a Reply