You are currently viewing Dkt. Samia: 2026 mwanzo utekelezaji wa dira
Dira mpya

Dkt. Samia: 2026 mwanzo utekelezaji wa dira

Rais Samia Suluhu Hassan amesema mwaka 2026, ndipo Tanzania inaanza utekelezaji wa Dira yake ya Taifa ya Maendeleo mwaka 2050.

Katika kipindi hicho, amesema Serikali itaendelea kutekeleza mkakati wa muda wa kati wa miaka mitatu (2025/2026 – 2027/2028).

Mkakati huo, amesema ni kuongeza mapato kwa kuimarisha matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika kukusanya mapato na kuongeza umakini kwenye usimamizi wa fedha na rasilimali za umma.

Rais Samia ameeleza hayo leo, Jumatano Desemba 31, 2025 katika hotuba yake kwa Taifa aliyoitoa akiwa Ikulu Ndogo ya Tunguu iliyopo Mkoa wa Kusini Unguja visiwani Zanzibar.

Leave a Reply