Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Aprili 16, 2025 amefika na kukagua eneo la Matandu na Somanga Mtama barabara kuu ya Dar es Salaam – Lindi yaliyokuwa yamekatika hivi karibuni kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani Kilwa Mkoani Lindi.

Katika Ziara hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa ameambatana na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, Waziri wa Ulinzi, Stergomena Tax, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Tellack pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini, Francis Ndulane.
Aprili 6 mwaka huu, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Lindi ulitangaza kusitisha matumizi ya barabara inayounganisha mikoa ya kusini kutokana na kukatika kwa daraja la dharura Somanga Mtama.