You are currently viewing Mastaa Barcelona, AC Milan wamiminika Tz kujivinjari

Mastaa Barcelona, AC Milan wamiminika Tz kujivinjari

Msimu mashuhuri wa utalii nchini umeanza kwa kasi na baada ya nyota wa zamani wa Man United na AC Milan @iamzlatanibrahimovic (wafuasi milioni 63 IG pekee) kutua nchini kutalii nyota wengine kadhaa wameonekana nchini wakivinjari maeneo mbalimbali. 

Miongoni mwao ni kiungo wa Barcelona ambaye pia huchezea Timu ya Taifa ya Hispania, Pedro González López, maarufu kama @pedri , ambaye ameshatua nchini na ameonesha picha akitua uwanja wa Kogatende, Serengeti.

Pamoja na kuchezea timu za vijana za Spain, mwaka 2022 Pedri alicheza mechi zote nne za nchi yake kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar kabla ya kuondolewa na Moroko. Huyu yupo nchini akiwa na wafuasi zaidi ya milioni 17 katika mtandao wa IG pekee. 

Serengeti pia na visiwa vya karafuu Zanzibar vimempokea mwanadada maarufu kwenye vituo vya TV za michezo Mashariki ya kati hasa nchini Misri, Mek Helmy, akitangaza radio kadhaa ikiwemo Al Masr na televisheni ya On Sport. 

Pamoja na Zanzibar na Serengeti @maihelmy.official (wafuasi milioni 8 kwenye IG pekee) pia amefanya zao jipya la utalii nchini la utalii wa kuruka kwa ndege na kuuona mlima Kilimanjaro kwa juu (scenic view).

Leave a Reply