Rais Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake imekubaliana kushirikiana na Misri katika kilimo cha mazao na mifugo ili kunufaika na soko la mataifa ya Afrika ambayo hutumia Dola za Marekani bilioni 70 kila mwaka kuagiza chakula kutoka nje.
Amesema Tanzania ina hekta 29 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na inashika nafasi ya pili kwa wingi wa mifugo, huku Misri ikiwa miongoni mwa nchi zilizopiga hatua katika teknolojia za umwagiliaji na uzalishaji wa mbegu.
Katika mazungumzo yao, amesema Misri imeonyesha nia ya kuwekeza katika kilimo na ufugaji na Ranchi ya Ruvu ndiyo itakayotumika.
Rais Samia ameyasema hayo leo, Jumamosi Julai 18, 2026 alipozungumza na wanahabari baada ya mazungumzo yake na Rais wa Misri, Abdel Fattah El-Sisi aliyepo nchini kwa ziara ya siku moja.
