Afisa wa polisi mlevi nchini Zambia amewaachilia washukiwa 13 kutoka kizuizini ili waende kusherehekea mwaka mpya.
Inspekta wa upelelezi Titus Phiri alikamatwa baada ya kuwaachilia washukiwa hao kutoka kituo cha polisi cha Leonard Cheelo katika mji mkuu, Lusaka.
Washukiwa hao 13 walishtakiwa kwa makosa ya uhalifu kama vile kushambulia, ujambazi na wizi. Kwa sasa wote hawajapatikana na msako umeanzishwa ili kuwatafuta.
Afisa huyo alifungua gereza la wanaume na wanawake na kuwaagiza washukiwa waondoke huku akisema wako huru kusherehekea kuingia mwaka mpya.
Taarifa ya polisi inasema, kati ya washukiwa 15 waliokuwa kizuizini, 13 walitoroka, na baada ya tukio hilo, afisa huyo alikimbia eneo la tukio, kabla ya kukamatwa.