Rais Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa amefanya uteuzi, uhamisho na mabadiliko ya viongozi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka miongoni mwa walioteuliwa ni pamoja na Godírey Eliakimu Mnzava, Afisa Tarafa ya Ilemela ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi.
Mzava ambaye alikuwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka jana, amechukua nafasi iliyoachwa wazi na James Wilbert Kaji aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wva Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).



