You are currently viewing Rais Dkt. Samia, Rais wa Angola wajadili hali ya usalama Kusini mwa Afrika

Rais Dkt. Samia, Rais wa Angola wajadili hali ya usalama Kusini mwa Afrika

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema amejadiliana na Rais wa Angola, Joao Goncalves Lourenco hali ya usalama na utulivu ndani ya eneo la kusini mwa Afrika ambapo
wamesikitishwa na hali iliyopo ya kuvunjika kwa usalama katika nchi kadhaa hasa Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pamoja na maeneo ya maziwa makuu.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es salaam leo, Oktoba 29,2026 ,baada ya mazungumzo na Rais wa Angola Joao Lourenco, Dkt Samia amesema wamejadiliana kuhusu namna yakusaidia juhudi za kutafuta amani kwenye migogoro inayoendelea kwenye ukanda wetu.

Rais Samia amesema amemwambia Rais Lourenco kuwa nafasi yake ya ukinara ya masuala ya afya ya mama na mtoto anayoyatumikia katika Umoja wa Afrika (AU) kama kinara wa afya ya mama na mtoto ambapo amemuomba aungane naye kwenye jitihada hizo.

Lakini pia wamezungumzia upande mwingine kuwa Angola wafuate ule mtindo wetu tuliouanzisha kama kinara wa AU wa ziro mama kufa wakati wakijifungua na ziro mtoto kufa wakati anazaliwa na kuwa na ziro mtoto ambaye hajachanjwa.