Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuhutubia leo, Novemba 11, 2026, Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), unaofanyika Antalya, Uturuki.
Rais Samia yupo Antalya kushiriki mkutano huo unaofanyika kuanzia Novemba 9 hadi 20, 2026, ukiwakutanisha viongozi wa nchi na Serikali kutoka sehemu mbalimbali duniani kujadili na kuendeleza hatua za kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
Miongoni mwa ajenda kuu za COP31 ni kuongeza upatikanaji wa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuimarisha ustahimilivu wa sekta muhimu za kiuchumi, kuendeleza matumizi ya nishati safi, hususan nishati safi ya kupikia, pamoja na kuharakisha utekelezaji wa Mkataba wa Paris kwa kushirikisha nchi zote, ikiwemo kuendeleza biashara ya kaboni.
Katika mkutano huo, Tanzania na Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC) zinatarajiwa kusaini makubaliano yatakayoweka msingi wa Tanzania kuwa mwenyeji wa mikutano mbalimbali ya UNFCCC itakayofanyika barani Afrika. Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza fursa za utalii wa mikutano, biashara, ajira na uwekezaji nchini.
#TanzaniaCOP31
