Rais Samia Suluhu Hassan, akiambatana na Rais wa Angola, João Manuel Gonçalves Lourenço, wanasafiri kwa treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma, ambako Rais Samia anatarajiwa kuzindua rasmi majengo ya ofisi za wizara na taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami katika Mji wa Serikali Mtumba.

Rais Lourenço yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, kuanzia Oktoba 28 hadi 30, 2026, yenye lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Angola.
Uzinduzi huo unafanyika leo, Oktoba 30, 2026, ukiwa ni hatua muhimu katika kukamilisha na kuanza kutumika kwa miundombinu ya Mji wa Serikali Mtumba, unaokusudiwa kuimarisha ufanisi wa shughuli za Serikali na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
