Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ipo tayari kwa maridhiano kwa kufuata njia sahihi na sio kupewa masharti ya nini cha kufanya ili kulifanikisha hilo.
Katika hoja yake hiyo, amewajibu wanaoweka masharti ya kinachopaswa kufanywa ili wakubali kukaa mezani, akisema Tanzania ni nchi huru inayoendesha mambo yake, hivyo haitashurutishwa na yeyote.
“Nimepata salamu za wengine wanaowapa nguvu kuwa hakuna mazungumza hadi huyu aachiwe au mfanye hili na hili… Serikali haipewi masharti hayo,” amesema Rais Samia.
Akionyesha dhamira ya maridhiano, mkuu huyo wa nchi amesema huu sio wakati wa kukaa na kunyoosheana vidole, bali kushikana mkono, kujenga umoja na kutumia njia sahihi kutatua changamoto zilizopo.
