Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kati ya asilimia 6.3 na 6.5 mwaka huu, baada ya kufikia asilimia sita mwaka jana na kuongoza nchi za Afrika Mashariki.
Amesema ukuaji huo ungeweza kuwa mkubwa zaidi kama kusingekuwa na changamoto zinazotokana na matukio mbalimbali yanayoendelea duniani.
Rais Samia ameyasema hayo leo, Ijumaa Novemba 20, 2026, wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika Chuo cha Polisi (CCP), Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Rais Samia amesema ukuaji wa uchumi nchini unaonekana pia kupitia kuongezeka kwa shughuli za biashara ndogo na za kati katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
“Hatukui tu katika karatasi za Wizara ya Mipango na Uchumi, lakini ukizunguka Tanzania unaona kabisa kuna ukuaji wa biashara ndogo na za kati. Uchumi wa nchi uko vizuri wananchi wana fedha mkononi isingekuwa hivyo biashara zile zisingekuwa,” amesema.
