You are currently viewing Rick Ross ampongeza Rais Samia kwa kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia
Rick Ross

Rick Ross ampongeza Rais Samia kwa kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia

Msanii wa miondoko ya Hip Hop kutoka Marekani, Rick Ross, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia, akisema muziki na vipaji na vinavyotoka nchini vinapaswa kupewa nafasi zaidi kimataifa.

Rick Ross amesema Tanzania imekuwa akilini mwake kutokana na kile alichokieleza kuwa ni vipaji ya muziki na nguvu kubwa inayotoka nchini, huku akitoa heshima kwa Rais Samia kwa mchango wake katika kuipeleka Tanzania kwenye jukwaa la kimataifa.

“Heshima kubwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia.” amesema katika ujumbe wake.

Msanii huyo pia ametaja uzuri wa Tanzania, akivitaja vivutio vya Serengeti na Zanzibar, huku akieleza kuwa yuko tayari kuitembelea nchi hiyo na kutumia muda kukutana na watu wake, kufahamu utamaduni wake na kupata uzoefu wa moja kwa moja.

Aidha, Rick Ross amesema yeye na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, wana mipango mikubwa ya kushirikiana na tasnia ya muziki Tanzania, ikiwamo kufanya kazi na baadhi ya wasanii wakubwa nchini pamoja na kuwafikia wasanii wa kizazi kipya.

“Kuna vipaji vya ajabu sana huko, na ninataka dunia ivione.” amesema, akisisitiza kuwa ushirikiano huo ndiyo kwanza unaanza.