You are currently viewing Saashisha Mafuwe aapa kutatua changamoto vyama vya ushirika wilayani Hai

Saashisha Mafuwe aapa kutatua changamoto vyama vya ushirika wilayani Hai

Mbunge wa Jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe ameapa kupambana na changamoto za vyama vya ushirika ambavyo vimekua ni kikwazo vya maendeleo katika wilaya hiyo.

Saashisha amebainisha hayo katika ziara yake aliyoifanya kwenye kata ya Narumu ambapo wananchi walionesha kuridhishwa na utekelezaji wa ahadi za rais ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya, shule na ujenzi wa barabara ambazo zimeleta urahisi wa usafiri kwa wananchi hao.

Aidha, wananchi katika jimbo hilo wameungana kumwombea Rais  Samia Suluhu Hassan huku wakiahidi kumpa kura za kishindo katika uchaguzi mkuu, kutokana na kazi alizozifanya katika jimbo hilo.

Leave a Reply