You are currently viewing Samia atuma salamu za rambirambi vifo vya wahudumu saba wa afya Kigoma

Samia atuma salamu za rambirambi vifo vya wahudumu saba wa afya Kigoma

Serikali inaomboleza vifo vya wafanyakazi saba wa afya waliofariki baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kupinduka kufuatia upepo mkali katika maji ya Ziwa Tanganyika siku ya Ijumaa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Rais, wahudumu hao wa afya walikuwa wakielekea katika kijiji cha Kagunga kilichopo mpakani mwa Tanzania na Burundi kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu kwa wananchi.

Rais Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kufuatia tukio hilo la kusikitisha, akieleza masikitiko yake makubwa na kuzipa pole familia za marehemu pamoja na sekta ya afya nchini.

Taarifa ya Ofisi ya Rais imeeleza kuwa taifa linaomboleza kupoteza wataalamu hao waliokuwa wakitekeleza jukumu muhimu la kuwahudumia wananchi, hususan katika maeneo ya pembezoni yenye changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya.

Leave a Reply