You are currently viewing Samia: Dabi ya Simba, Yanga kuongeza hamasa Kizimkazi Festival

Samia: Dabi ya Simba, Yanga kuongeza hamasa Kizimkazi Festival

Rais Samia Suluhu Hassan amesema mchezo wa dabi kati ya Simba na Yanga utakaochezwa katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar, utaongeza hamasa na mvuto wa Tamasha la Kizimkazi linalotarajiwa kuanza kesho.

Simba na Yanga zitakutana Agosti 12, 2026 katika mchezo wa Ngao ya Jamii, siku ambayo pia Tamasha la Kizimkazi litazinduliwa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo matembezi ya pamoja na uzinduzi wa miradi ya maendeleo.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Agosti 11, 2026, alipokuwa akizungumza na wananchi katika Maskani ya Kisonge, Zanzibar, akieleza kuwa mchezo huo utachangia kuvutia zaidi washiriki na wageni wa tamasha hilo.

“Tunawapongeza, kesho wanakuja kufanya dabi hapa kuunga mkono Kizimkazi Festival. Dabi linakuja kupigwa kesho hapa Zanzibar,” amesema.