Rais Samia Suluhu Hassan, amesema miradi ya maendeleo inayotekelezwa nchini ni fursa muhimu kwa wananchi katika kukuza uchumi na kuboresha ustawi wao.
Amesema Serikali inaendelea kuwekeza katika miradi mbalimbali kwa lengo la kusogeza huduma muhimu karibu na wananchi, kufungua fursa za kiuchumi na kuongeza ustawi wa jamii.
Akizungumza na wananchi wa Kizimkazi leo Agosti 13, 2026 Rais Samia amewataka wananchi kutunza miundombinu ya miradi hiyo, akisisitiza kuwa inatumia fedha nyingi na inapaswa kunufaisha kizazi cha sasa na kijacho.
“Ni wajibu wetu na lazima ndugu zangu tuitunze miradi hii. Kama tunavyotazama kwa macho yetu, tuitunze miradi hii,” amesema.
Aidha, Rais Samia amewahimiza wananchi kudumisha amani, akisema amani ndiyo msingi unaowezesha Serikali kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo.
