You are currently viewing Samia: Toeni haki kwenye migogoro ya wafanyakazi, epukeni upendeleo

Samia: Toeni haki kwenye migogoro ya wafanyakazi, epukeni upendeleo

Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi wa Migogoro ya Kazi (CMA) kutekeleza majukumu yao kwa umakini, uadilifu na kuzingatia sheria bila kuongozwa na chuki wala upendeleo.

Dkt Samia ameeeleza hayo leo Jumatatu Novemba 2,2026 wakati akiwaapisha viongozi hao wateule, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa Dkt Samia, watendaji wa kazi CMA yao ni ngumu ya kushughulikia migogoro ya wafanyakazi ambayo mwisho wa siku inapelekwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi, kisha kwa Rais.

“Naletewa mashtaka mliotoa uamuzi na wakati mwingine wasioridhika wanakata rufaa, kwa hiyo naletewa rufaa zao pia. Rufaa zingine naambiwa nizikatae kwa sababu hawana hoja kupinga maamuzi ya Tume na zingine nizikubali,kwa sababu wana hoja,” amesema.

Amesema hatua hiyo, inaonesha umuhimu wa viongozi hao kufanya kazi kwa umakini na kuzingatia viapo walivyoapa vya kutenda haki bila chuki wala upendeleo, akisisitiza mfanyakazi anapokosea anapaswa kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za kazi.