You are currently viewing Samia: Tuitumie stendi kujinufaisha kiuchumi

Samia: Tuitumie stendi kujinufaisha kiuchumi

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema ni muhimu wananchi wa Hanang, mkoani Manyara, wakaitumia stendi yam abasi iliyojengwa kujinufaisha kiuchumi.

Dkt Samia ameeleza hayo, leo Ijumaa Oktoba 3, 2025 alipozungumza na wananchi wa Hanang, mkoani Manyara, katika ziara yake ya kampeni za urais.

Amesema stendi hiyo haipaswi kutumiwa na wananchi kupanda na kushuka kutoka kwenye magari pekee, bali waanzishe biashara na hatimaye kunufaika kiuchumi. 

Dkt Samia ameeleza stendi hiyo inayofungua fursa za kibiashara kwa wananchi wa Hanang, akiwasihi waitumie kufanya biashara na kukuza uchumi.

Leave a Reply