You are currently viewing Samia: Tuvunje makundi, tusiishiwe ‘pawa’

Samia: Tuvunje makundi, tusiishiwe ‘pawa’

Mgombea wa urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka wanachama wa chama hicho mkoani Iringa, wavunje makundi yaliyosababishwa na michakato ya uteuzi wa ndani, ili kwenda kwenye uchaguzi wakiwa wamoja.

Katika kuijenga hoja hiyo, Dkt Samia ametumia sehemu ya wimbo wa Msanii wa kizazi kipya, Mbosso, ‘Pawa’, akisema kuendelea kuwa na makundi, chama hicho kitakwenda kwenye uchaguzi kikiwa kimeishiwa pawa.

Wimbo huo ulioteka mioyo ya washabiki wengi wa muziki wa kizazi kipya, maudhui yake yanalenga kuonyesha namna mtu alivyoishiwa nguvu ‘pawa’ kwa sababu ya mapenzi.

Dkt Samia ametoa ujumbe huo, leo Jumamosi Septemba 6, 2025 alipozungumza na wananchi wa Mafinga mkoani Iringa katika mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni za urais.

“Tuvunje makundi ili tuende kwenye uchaguzi tukiwa wamoja, chama kikiwa na nguvu. Tusiishiwe ‘pawa’ kama walivyoishiwa wenzetu. Twende tukiwa na nguvu kama chama kimoja, Chama Cha Mapinduzi,” amesema na kushangiliwa na maelfu ya wananchi waliokuwa wakimsikiliza.

Leave a Reply