Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Tanzania imeiomba Kampuni ya Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika ya Mashariki (EACOP) idumishe utaratibu wa kutoa mafunzo ya juu elimu kwa Watanzania ili taifa liwe na hazina ya wazawa wenye uwezo wa kusimamia na kuendeleza sekta ya gesi na matufuta.
Akitoa ombi hilo wakati wa uzinduzi wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 12 watakaosoma progamu za nyanja za mafuta, gesi na viwanda vya uchimbaji, Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Elimu, Saiyansi na Teknolonia, Profesa Daniel Mushi, alisema EACOP imedhihirisha dhamira ya kugharamia elimu kwa Watanzania ili wawe wajuzi katika sekta ya gesi na mafuta.
“Ombi letu waendelee na utaratibu huu ili tuwe na idadi kubwa ya watu wa aina hii wenye uwezo wa kusaidia kuendeleza raslimali tulizonazo. EACOP wana mashirikiano na vyuo vya VETA, wanafundisha watu kazini, hands-on training, wamejenga chuo cha gesi na mafuta, wanandaa internship programmes, wanawapeleka nje watu wetu ili wapate ujuzi waweze kusimamia sekta ya gesi na mafuta. Tunaomba waendelee na utoaji wa skolashipu hizi,” alisema Profesa Mushi.
Programu sita za scholarship 12 za udhamini zinagharamiwa na Daqing Oilfield Construction Group Ltd (DOCG), kila programu ikiwa na wanafunzi wawili. DOCG ni mkandarisi wa EACOP anayejenga temino ya mafuta Tanga.
Profesa Mushi alieleza kuwa waombaji walikuwa 501, wakachujwa kwa vigezo vya uwezo wa kitaaluma na kubaki 12.
Alisema baadhi ya waombaji walikua wahadhili kutoka vyuo vikuu vya Dar es Salaam, Mbeya na DIT.
Alieleza kuwa wahitumu wanatarajiwa wasimamie uendeshaji wa mradi na wengine wanaweza kuwa wafundishaji katika vyuo (academic staff) nchini, na kuongeza kwamba mradi huu utagharimu milioni laki tatu na sita (306,000m/-) au dola za Marekani 116,000.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam (Taaluma), Profesa Bonaventure Rutinwa, ameahidi kwamba chuo chao kitatoa ushirikiano mkubwa ili kufanikisha programu hizo sita.
“Mradi huu umeanzishwawadau makubwa katika bomba la mafuta ili kuendeleza raslimali watu hapa Tanzania. Tanawashukuru kuanza na chuo Dar es Salaam, wamechagua sehemu sahihi. Tuko tayari kuwapa ushirikiano kadri itakavyohitajika,”aliahidi.
Meneja wa Tawi DOCG, Tanzania, Chu Dayong, alisema wanajivunia ushirikiano baina yao na UDSM, na kueleza kuwa programu hizo sita zinafungua milango kwa Watanzania wenye vipaji kupata elemu ya juu katika nyanja ambazo ni muhimu kwa uchumi wa baadaye wa Tanzania.
Aidha, alieleza, wahitimu watapewa kipaumbele cha ajira za baadaye katika tasinia ya mafuta na gesi ambako watashiriki kutatua changamoto halisi katika tasinia hiyo.
Meneja wa EACOP wa Sera ya Ushirikishaji na Uwezeshaji Wazawa, Neema Kweka, alieleza kuwa programu hizi ni mwendelezo wa EACOP wa utekelezaji wa sera ya ushirikishaji na uwezeshaji wazawa nchini Tanzania.
Alitoa mifano ya kwamba Watanzania wamepelekwa China, UAE, Singapore, Afrika ya Kusini, Italia, Spain, Misri, Omani na Ufaransa kwa mafunzo ya usambazajina utoaji wa huduma.
Aidha, Watanzania 50 tayari wamepewa mafunzo ya ukufunzi na kuongeza kwamba EACOP imekuwa na ushirikiano wa kuboresha miundombini ya vyuo, kwa mfano Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Arusha Technical School, VETA Moshi, VETA Shinyanga, VETA Tanga na Chuo cha Bandari.
Mradi wa bomba unaanzia Wilaya ya Hoima, Uganda na kuishia Ras ya Chongoleani, Tanga.