Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga Sh bilioni 43 ili kuimarisha michezo katika shule mbalimbali nchini na kati ya hizo, sh. bilioni 32 ni kwa ajili ya kuimarisha Chuo cha Michezo Malya.
Ametoa kauli hiyo Juni 9, 2025 wakati akifungua mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari Tanzania (UMITASHUMTA na UMISSETA) kwenye viwanja vya Kichangani vilivyoko Kihesa, mkoani Iringa.
Akielezea mikakati ya Serikali ya kuendeleza michezo na sanaa nchini, Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuimarisha Chuo cha Michezo Malya ili kiendelee kutoa mafunzo kwa kuzingatia utaalam na kuimarisha ufundishaji wa masomo ya michezo shuleni.