Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba, amewasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali ya shilingi trilioni 56.49 kwa mwaka 2025/26.
“Makadirio ya matumizi ya Serikali ya shilingi trilioni 56.49 kwa mwaka 2025/26 yanajumuisha: Stahiki za watumishi na michango ya pensheni (Serikali Kuu) shilingi trilioni 9.17;
“Ununuzi wa bidhaa na huduma shilingi trilioni 5.58; malipo ya riba za mikopo shilingi trilioni 6.49; na ruzuku (subsidies & transfers) kwa taasisi za Serikali, mashirika ya umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa shilingi trilioni 22.17.
“Aidha, Serikali inatarajia kutumia shilingi trilioni 7.72 kugharamia malipo ya mtaji kwa deni la ndani na nje,” amesema Waziri Nchemba.